Wakazi wa lokesheni ya Mwamonari, eneo bunge la Kitutu Chache Kaunti ya Kisii amewaonya wakazi ambao hawahudhurii vikao vya mabaraza na kusema watachukuliwa hatua kali ya kisheria.
Wito huo umetolewa baada ya kikao cha baraza kuandaliwa eneo la Motari siku ya Jumatano na idadi ndogo kujitokeza, jambo ambalo lilimkera chifu wa eneo hilo na kutoa onyo kali kwa wale ambao hususia kuhudhuria vikao hivyo.
Akizungumza siku ya Jumatano katika kikao hicho cha baraza kilichoandaliwa, Titus Mochiemo aliomba kila mkazi wa lokesheni yake kuhudhuria vikao vya mabaraza kujua mengi haswa katika usalama na maendeleo mengine.
"Ninapoita wakazi kwa baraza nina mengi ya kuwaeleza, wale wako hapa mnapoondoka mwambile wale hawakuhudhuria kikao cha leo wasirudie tabia hiyo na wawe wanakuja kwa mabaraza kama si hivyo hatua itachukuliwa dhidi yao,” alisema chifu huyo.
Wakati huo huo, Chifu huyo aliomba wanachama wa polisi jamii waliochaguliwa hivi maajuzi kufanya kazi yao inavyostahili na kuweka usalama vijijini, ila aliwaonya kutotumia nguvu kama maafisa wa polisi.
Pia alionya wale ambao huendesha wizi katika lokesheni hiyo na kuwaonya kuwa siku zao zinahesabiwa huku akiomba wazazi kuwachukua wanao shuleni na kupokea elimu kwani masomo ni ya bila malipo.