Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Usimamizi wa chuo kikuu cha ufundi cha Mombasa unatarajia kufungua tawi jingine la chuo hicho katika kaunti ya Kilifi.

Kauli hii ilitolewa siku ya Alhamisi na naibu chansela wa chuo hicho Prof Josphat Mwatela, na kusisitiza kuwa tawi hilo litaanza kufunza masomo ya ubaharia.

Mwatela aliongeza kuwa kutokana na kuwepo kwa bahari jijini, basi mafunzo hayo yatasaidia hasa wanafunzi wanaonuia kusoma taaluma hiyo.

Mwatela aliyasema haya kwenye hafla ya kufunzu mahafala wa chuo hicho, ambapo mahafala zaidi ya mahafala elfu moja na mia saba walifuzu kwa daraja mbali mbali katika chuo kikuu cha ufundi Mombasa.

Na Kwa mara ya kwanza tangu chuo hicho kupandishwa daraja na kuwa chuo kikuu, wanafunzi saba wamefuzu kwa shahada ya uzamifu.