Baraza la Maimamu na Wahubiri wa humu nchini CIPK limewataka viongozi wa makundi ya vijana yanayolenga kuzua vurugu kwa misingi ya kutetea raslimali zao na ardhi ya Wapwani kujadiliana vyema na serikali ili kuzua migogoro ya kudumisha amani.
Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Sheikh Mohammed Khalifa alisema kuwa njia pekee ya kusuluhisha matatizo ni kupitia kwa mazungumzo na idara husika serikalini ili kuhakikisha kuwa wakazi wanaishi bila hofu ya kiusalama.
Akizungumza mjini Mombasa siku ya Alhamisi, Sheikh Khalifa alisema kuwa makundi mengi yanayozua vurugu hususan wakati taifa hili linapokaribia kufanya uchaguzi mkuu huchochewa na baadhi ya viongozi wa kisiasa na akawataka vijana kujiepusha viongozi kama hao.
“Tunawaomba vijana kuwa watulivu na kujitenga na baadhi ya watu fulani wanaolenga kuwagonganisha vijana kuzua vuugu watakati taifa hili linakaribia uchanguzi mkuu, la msingi ni kufanya mazungumzo na idara husika,” alisema Sheikh Khalifa.
Wakati uo huo walishtumu viongozi wa kisiasa wanaowachechea vijana kuzua vurugu na kuharibu usalama wa eneo hili kwa misingi yao binafsi ya kujinufaisha kisiasa akiwataka kukoma mara moja ili Wakenya waishi kwa amani.
Tunaomba viongozi wa kisiasa kukoma mara moja kutowagonganisha vijana kuharibu usalama wa eneo hili kwani usalama wa eneo la Pwani na Kenya kwa jumla ni muhimu kwa Wakenya na wala sio kwa baadhi ya watu fulani,” aliongeza Sheikh Khalifa.