Mwenyekiti wa ODM Nakuru Denis Okomol amewasuta wapizani wa mrengo wa Cord wanaodai viongozi wa CORD watatengana ifikapo mwaka ujao.
Katika kikao na wanahabari mjini Nakuru,Okomol alisisitiza kwamba vinara hao ni marafiki wa dhati na kamwe hawatatengana bali wataunga mkono mmoja wao katika kuwania urais mwaka 2017.
''Kuna baaadhi ya watu wameanza kueneza uvumi eti vinara wenza wa CORD watagawanyika mwaka ujao, kile ambacho hawajui ni kwamba watatu hawa ni marafiki na ikifika 2017 wataunga mkono mmoja wao kuwania urais,'' Okomol alisema.
Wakati huo huo akizungumzia swala la ardhi huko Mombasa, Okomol aliitaka serikali kukoma kutumia changamoto ya ardhi Lamu kujipatia umaarufu.
''Ni jambo la kusikitisha mno kwamba serikali inatumia swala la ardhi huko pwani kujipa umaarufu kisiasa ilhali maskowta wanaendelea kuteseka,'' Okomol alisema.