Muungano pinzani wa Cord umeapa kushinikiza kufanyika kwa kura ya maamuzi ya OKOA Kenya kabla ya mwezi Julai mwaka huu.
Kinara wa Cord Raila Odinga alisema siku ya Jumapili huko Ukunda, kuwa muda wa tume ya uchaguzi IEBC kukagua sahihi milioni 1.4 zilizokusanywa na Cord zinakamilika juma lijalo, lakini tume hiyo haijaonyesha mwelekeo wowote.
Odinga alionyeshwa kushangazwa na tume hiyo kudai kwamba haina fedha za kutosha ni njama ya kuhujumu kufanyika kwa kura ya maamuzi na kwamba kamwe Cord hawatakubali.
Aidha, aliitaka tume hiyo kuharakisha ukaguzi wa sahihi hizo ili mswada wa kufanyika kwa kura ya maamuzi uweze kufikishwa katika mabunge ya kaunti.