Muungano pinzani wa Cord umetakiwa kushirikiana na serikali ili kutafuta suluhu la kudumu katika matatizo yanayowakumba wananchi.
Akizungumza mjini Mombasa siku ya Ijumaa, Gavana wa Machakos Alfred Mutua amewataka viongozi kutoka mrengo pinzani kukoma kuinyoshea Jubilee kidole cha lawama bali kushirikiana katika kutekeleza maendeleo ya taifa.
Akiongea kwenye ufunguzi wa afisi ya Maendeleo Chapchap katika eneo la Changamwe, Mutua amewataja viongozi wa Cord kuwa na ubinafsi na lengo lao kuu ni kujinufaisha wao kibinafsi huku wakiwasahau wananchi mashinani.
Aidha, amewalaumu viongozi waliokuwa katika serikali na kushindwa kufanya maendeleo huku kwa sasa wakiwa mstari wa mbele kushtumu uongozi wa rais Uhuru Kenyatta.