Share news tips with us here at Hivisasa

Mtu mmoja ameuwawa kwa kupigwa risasi katika mzunguko wa barabara ya Jomo Kenyatta Avenue eneo la Lebanon karibu na Kanisa la Mombasa Pentecostal Church mjini Mombasa Jumatano jioni.

Kulingana na waliyoshughudia tukio hilo, watu wawili waliokuwa wameabiri pikipiki walifika eneo hilo na kumfyatulia risasi mara mbili kichwani dereva wa tuk tuk na kumuuwa papo hapo kisha wakatoweka.

Haijabainika wazi kiini cha mauaji hayo kilisababishwa na nini kwani genge hilo linalokisiwa kuwa la majambazi, hawakumuibia chochote dereva huyo.

Tukio hilo ni la pili kutokea katikati mwa mji wa Mombasa chini ya juma moja tu ambapo dereva mwingine wa tuktuk aliuwawa kwa kudungwa kisu na kundi moja la vijana katika eneo la Bunley huko Majengo mjini Mombasa.

Mwili wa mwendazazke umepelekwa katika hifadhi ya maiti katika hospitali kuu ya ukanda wa pwani.

Hata hivyo afisa mkuu wa Polisi Kisiwani Mombasa Martin Asin amethibitisha kisa hicho na kusema kwamaba uchunguzi umeanzishwa kuhusu tukio hilo.