Wakristo wote wamehimizwa kueneza ujumbe wa wananchi kujisajili kama wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza Jumapili wakati wa ibada katika kanisa la PCEA Dr Arthur mjini Nakuru, mchungaji James Mwangi alisema kuwa kuna umuhimu wa wakristo kuendeleza ujumbe huo ili kuhakikisha kila mwananchi anajisajili kama mpiga kura. 

Kwa mujibu wake, swala hilo halifai kuachiwa wanasiasa pekee, bali ni wajibu wa kila mmoja. 

"Tusiwaachie tu wanasia pekee bali nawaomba wakristo pia tuhakikishe kuwa tunaeneza habari hizi za kusajiliwa wapiga kura," alisema Munene. 

Isitoshe, ametoa wito kwa akina mama na vijana wasio na vitambulisho kufanya hima kabla ya uchaguzi mkuu ujao. 

Wakati huo huo, ametoa wito kwa serikali kuhakikisha kwamba hata wafungwa wanapata haki ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa 2017. 

Ikumbukwe kuwa zoezi hilo la kusajili wapiga kura liling'oa nanga Februari 15 na litatamatika Machi 15.