Share news tips with us here at Hivisasa

Naibu wa rais William Ruto amesema kuwa serikali imehakikisha Elimu kwa watoto imepewa kipao mbele na kuwa  usawa katika utoaji wa huduma kwa wananchi itazingatiwa.

Ruto alisema kuwa ni kutokana na hilo serikali imeongeza kiwango cha fedha katika shule za msingi na upili na kutupilia mbali malipo ya fedha za mitihani ili kuhakikisha kuwa watu wote wananufaika na elimu. 

Naibu wa rais alijumuika  na wanafunzi wa msingi katika shuleya Lelu.

"Serikali iko imara kusambaza umeme kwa kila shule nchini mwishoni mwa mwezi huu, elimu ni lengo letu," Ruto alisema.

Aliongeza kuwa serikali itatoa vifaa vya afya katika hospitali ya kaunti ya Kericho na ile ya Sigowet vitakavyogharimu shilingi milioni 420 namilioni 380 mtawalia.