Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Eneo la Likoni, Kaunti ya Mombasa linaongoza kwa visa vya ubakaji vya watoto walio na umri chini ya 14 huku kati ya watoto watatu hadi wanne wanabakwa kila mwezi na hata visa vingine kutoripotiwa.

Haya ni kwa mujibu wa mwanaharakati wa Sauti ya wanawake eneo la Likoni Amina Juma akiongea siku ya Alhamisi katika eneo la Likoni jijini Mombasa.

Amina aliitaka idara ya mahakama iwape washukiwa hao dhamana kubwa kwani mara kwa mara jamaa hao huwa huru pindi tu baada ya kukamatwa, hali aliyoitaja kama kutatiza haki ya waathiriwa.

Aidha, ameongeza kuwa sharti idara hiyo ichukue muda mfupi kwa kesi hizo kwani waathiriwa huchoka kutafuta haki pindi kesi hizo zinapochukua muda mrefu.

Kisa cha hivi majuzi cha kuhuzunusha ni cha kubakwa hadi kufariki kwa mtoto wa miaka 13 katika eneo hilo la Likoni.

Katika ripoti ya Kituo cha Kitaifa cha utafiti wa uhalifu iliotolewa Aprili 2015, Kaunti ya Mombasa inaongoza kwa visa vya ubakaji wa watoto ikiwa na asilimia 60, ikifuatwa na kaunti ya Machakos na aslimia 58.3, huku huku kauniti ya Nyeri ikiandikisha visa vidogo kabisa ikiwa na asilimia 17.5.