Huku ulimwengu ukiendelea kuadhimisha siku ya saratani duniani, gavana wa Kaunti ya Nyamira John Nyagarama aliadhimisha siku hii kwa kupokeza mama mlemavu machela nje ya afisi yake. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Akihutubia wanahabari baada ya hafla hiyo siku ya Alhamisi, Gavana Nyagarama alisema ilimlazimu kuchukua hatua hiyo baada yake kugundua Yucabeth Nyamusi hakuwa na uwezo wa kutembea. 

"Nimeona ni vizuri kumsaidia mama huyu baada ya kugundua kwamba amekuwa akipitia masaibu mengi kwa kukosa machela ya kumwezesha kutembea." alisema Nyagarama. 

Gavana Nyagarama aidha aliwahimiza wahisani katika jamii kujitokeza kusaidia watu walio na matatizo kama haya. 

"Ni himizo langu kwa wahisani hasa wale walio na uwezo katika jamii kujitokeza kuwasaidia watu walio na changamoto sawia na hizi," aliongezea Nyagarama.