Viongozi wa serikali ya Kaunti ya Nakuru wamepongeza wakazi wa Njoro kwa namna walivyosuluhisha mzozo uliotokana na wizi wa mifugo walioibwa na watu wasiofahamika katika maeneo ya Ndefo na Chebitet.
Gavana Kinuthia Mbugua, aliyeongoza viongozi wengine katika kutoa pongezi hizo siku ya Ijumaa, alisema wakazi hao wanastahili kusalia na amani huku polisi wakitafuta suluhu kwenye tatizo hilo.
Wakazi wa Ndefo walikuwa wamefunga barabara ya Njoro-Mau kuelekea Narok wakitaka haki kutendeka baada ya mauaji ya Mzee Moses Njenga aliyeshambuliwa na wahalifu nyumbani kwake na kudungwa kwa mshale.
Mbugua akiwa pamoja na mbunge wa Njoro Joseph Kiuna walituliza umati huo wa watu kwa ahadi kwamba wahusika watakamatwa
“Hatufai kukubali mtu mmoja ama kikundi cha watu fulani kutugawanya kwa misingi ya kikabila,” alisema Mbugua.