Share news tips with us here at Hivisasa

Gavana wa kaunti ya Nakuru Kinuthia Mbugua amepuzilia mbali madai ya kuwa hospitali ya Njoro haina madawa.

Akiongea wakati alizuru kaunti hiyo ndogo, Mbugua amesema kuwa kuna baadhi ya watu ambao wanaeneza porojo za kisiasa.

“Kuna watu ambao hawatutakii mazuri kama kaunti. Kila wakati wanakosoa kwa sababu hawatakai maendeleo,” Mbugua alisema.

“Nataka wakazi wajue kuwa hizi ni propaganda na porojo za siasa,” Mbugua aliongeza.

Gavana huyo alisema kuwa serikali yake imekuwa ikitoa madawa kwenye hospitali zote za kaunti ya Nakuru ili kuhakikisha wakazi wanapata huduma zifaazo.