Gavana wa Kaunti ya Nakuru Kinuthia Mbugua, amewataka wanaharakati kumuheshimu na kukoma kutumiwa na wanasiasa kupinga uongozi wake.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kupitia taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari siku ya Jumanne, Mbugua aliwashtumu wanaharakati waliongoza maandamano kuelekea afisini mwake na kuwataka kuuheshimu utawala wake.

"Ni masikitiko kuona wanaharakati wakitumiwa na baadhi ya wanasiasa kufanya maandamano yasiyo na maana na kujaribu kuleta vurugu," ilisema taarifa hiyo.

"Ofisi yangu iko wazi kwa kila mkazi wa Nakuru lakini sitakubali wavunja sheria kuvuruga shuguli za serikali yangu maanake kuna njia mwafaka ya kuwasilisha malalamishi," taarifa hiyo ilisema.

Aidha, taarifa hiyo ilikanusha madai ya wanaharakati hao kuwa ufisadi umekithiri katika serikali ya Kaunti ya Nakuru.

"Kama wanaharakati wana ushahidi wa pesa kuporwa basi wacha waeende kwa tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC, badala ya kuleta fujo sizizo maana," ilisema taarifa hiyo.