Hatimaye bunge la kaunti ya Nyamira limefunguliwa baada ya miezi miwili unusu kwenye likizo.
Akihutubu wakati wa ufunguzi rasmi wa bunge hilo siku ya Jumanne, Gavana Nyagarama alisema serikali yake imeweka mikakati ya kuhakikisha utoaji huduma kwa wananchi ni huru na wazi.
"Utoaji huduma kwa wananchi ni mhimu sana katika ustawishaji wa maendeleo, na kwa maana hiyo nimeweka mikakati ya kuhakikisha huduma hizo kwa wananchi ni za usawa na wazi," alisema Nyagarama.
Nyagarama aidha aliwaomba wawakilishi wadi wa bunge hilo kuidhinisha kwa haraka miswada mhimu ili kustawisha maendeleo Nyamira.
"Nyinyi wawakilishi wadi mna wajibu wa kuhakikisha kuwa mnaidhinisha miswada mhimu kwa wakati unaofaa ili kustawisha maendeleo huku Nyamira," aliongezea Nyagarama.