Gavana wa kaunti ya Nyamira John Nyagarama amewapa changamoto vijana katika kaunti ya Nyamira kuhakikisha kwamba wanatumia vizuri shillingi millioni 30 zilizopokezwa wizara ya masuala ya vijana katika kaunti hiyo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akihutubia wakazi wa Bonyamatuta siku ya Jumamosi, Nyagarama alisema asilimia kubwa ya vijana wameshindwa kutambua miradi mhimu itakayo wawezesha kufadhiliwa, huku akiwahimiza kuhakikisha kuwa wamejiunga kwenye makundi ili kupokea ufadhili.

“Serikali yangu ilikuwa imepokeza wizara ya vijana na spoti shillingi millioni 30 ili kuwasaidia vijana kujiendeleza, ila nimesikia kwamba vijana hawajajitokeza kutumia vizuri pesa hizo,” alisema Nyagarama.

Gavana huyo aidha aliongeza kusema kuwa pesa hizo hazikuwa tu zimetengwa ili kufadhili tu miradi ya kispoti, bali zinaweza pia kuwasaidia wafanyabiashara wanaotaka kustawisha biashara zao.

“Tumekuwa tukifanya vizuri kwenye fani mbalimbali za kispoti ila changamoto ni kwamba hatujapata wanabiashara wanaojitokeza kujisajili ili biashara zao ziweze kupokea ufadhili, na ni himizo langu kwao kujitokeza ili kupokea ufadhili,” aliongezea Nyagarama.