Mbunge wa eneo bunge la Mugirango magharibi James Gesami amewapongeza wanafunzi waliofanya vyema kwenye mtihani wa kidato cha nne mwaka jana katika kaunti ya Nyamira.
Akihutubu mda mchache baada ya waziri wa elimu nchini Fred Matiang'i kutangaza wazi matokeo ya mtihani huo, Gesami aliwapongeza wazazi na walimu kwa ushirikiano mzuri ambao uliozalisha matokeo mazuri kwenye mtihani huo wa KCSE.
"Wakazi wa Nyamira kwa hakika nimefurahi sana kwa matokeo mazuri ambayo baadhi ya shule zetu za upili zimedhihirisha, na kwa kweli hizi sherehe zote ambazo tumezishuhudia ni ishara wazi kwamba wanafunzi wetu walitia bidii masomoni," alisema Gesami.
Gesami aidha aliongeza kusema kuwa matokeo hayo mazuri ya kidato cha nne yalitokana na ushirikiano wa walimu wazazi pamoja na wanafunzi.
"Ninamshukru Mungu kwa rehema zake, wazazi walimu na wanafunzi pia kwa ushirikiano mzuri," aliongezea Gesami.