Mtangazaji wa kituo cha radio kinachotangaza lugha ya kwanza Egesa fm Petronira Getena ameonyesha azma ya kukiwania kiti cha uwakilishi wa wadi, Nyatieko kaunti ya Kisii katika uchaguzi ujao.
Azimio hilo limekuja baada ya wengi wa wakaazi wa wadi hiyo kumtaka awe kiongozi wao kupitia maendeleo anayoyafanya katika eneo bunge la Kitutu Chache kusini kaunti hasa, wadi ya Nyatieko kwa kuandaa kombe mbalimbali za mipira ya kandanda ili kukuza talanta za vijana.
Akizungumza siku ya Jumapili, wakati finali za kombe aliloliandaa lilikuwa likichezwa, Getena alisema baadhi ya viongozi walio kwa viti hawatumii mamlaka yao kuwasaidia vijana na hata wakaazi kimaendeleo.
Getena amebuni umaarufu katika eneo bunge la Kitutu Chache kusini na katika wadi ya Nyatieko kwa kuandaa vikombe kadhaa ili kuwasaidia vijana kujiendeleza kupitia talanta zao.
“Baadhi ya viongozi hawafiki vijana karibu ili kutoa usaidizi, nilimwalika mwakilishi wa wadi hii ya Nyetieko Vincent Okenye kuhudhuria finali za kombe langu na hakuhudhuria mkitaka kuamua si mtaamua kunavyostahili ili tuone jinsi ya kusuguma gurudumu la maendeleo pamoja? Naomba tuwe pamoja mnapoendelea kuamua tubadilishe uongozi,” alisema Getena.
Aidha, mwanasiasa Nyandoro aliyehudhuria finali za kandanda hiyo alimuunga mkono mtangazaji Getena kukiwania kiti cha uwakilishi wadi kwani ameonyesha yale atayafanya anapochaguliwa katika mamlaka.
“Mtangazaji Getena hana mamlaka yoyote ya uongozi kwa sasa lakini mnayaona yale anayafanya wacha tuamue tmara moja tubadilishe uongozi wa wadi hii tumuunge mkono ili mumchague kama kiongozi wenu katika wadi ya Nyatieko,” alisema Nyandoro.