Share news tips with us here at Hivisasa

Mbunge wa Nakuru  Mashariki David Gikari amesema yuko tayari kuinua maisha ya vijana katika eneo bunge hilo .

Akizungumza katika uwanja wa Kamkunji Green stadium aliposhuhudia michuano ya robo fainali ya soka ya Nakuru Town East Interestates, Gikaria amewataka vijana kutumia vyema talanta walizo nazo.

Aliongeza kuwa kaunti ya Nakuru ina talanta na vipaji mbalimbali ambavyo vinafaa kukuzwa.

"Vijana wana talanta hapa na lazima tuwasaidie kuzikuza," Gikaria alisema.

Michuano hiyo inayofadhiliwa na afisi ya CDF ya eneo bunge hilo inatarajiwa kukamilika mwezi Disemba.

 Wakati huo huo,Mbunge Gikaria alitoa wito wa amani hasa katika mpaka wa kaunti za Nakuru na Narok.