Share news tips with us here at Hivisasa

Mbunge wa Nakuru mjini David Gikaria amewarai walimu wote katika kaunti ya Nakuru kuunga mkono serikali ya Jubilee kwenye uchaguzi ujao.

Akizungumza Jumanne, Gikaria alisema kuwa walimu wamehangaika mno mikononi mwa aliyekuwa waziri wa elimu Jacob Kaimenyi na wakati ni sasa wa swala hilo kutatuliwa.

"Rais wetu Uhuru Kenyatta pamoja na makamu wake William Ruto mbeleni walikuja wakadanganywa na jamaa mmoja anaitwa Kaimenyi....si mnamjua?na hata alituletea shida bunge lakini si rais alimtoa yeye kwa sababu alikuwa anadanganya rais kuhusu mambo yenu walimu,"Gikaria alisema.

Mbunge huyo alisema tayari kamati maalumu ya kushughulikia mishahara ya walimu imebuniwa na rais.

"Hivi karibuni rais amebuni kamati ya kushughulikia mishahara ya walimu na tunatumai maneno ya migomo imeisha," Gikaria alisema.