Share news tips with us here at Hivisasa

Hati miliki za ekari 350,000 zilizopatikana kinyume cha sheria kaunti ya lamu zimefutiliwa mbali na kuwekwa chini ya uongozi wa kaunti hiyo.

Hii ni baada ya waziri wa ardhi Jacob Kaimenyi kutangaza agizo hilo hapo jana jioni wakati wa mkutano wa Rais na viongozi wa kaunti hiyo .

Kaimenyi alisema kuwa ardhi hizo ni miongoni mwa sehemu 12 za ardhi zilizopewa ilani ya kufutiliwa mbali na tayari muda wa ilani hiyo ulikuwa umetamatika.

Waziri Kaimenyi anahoji kuwa serikali inapanga kufutilia mbali hati miliki zote zilizopatikana kinyume cha sheria na badala yake kuregeshewa wananchi wafanye ukulima na miradi mingine ya maendeleo.