Share news tips with us here at Hivisasa

Mwenyekiti wa chama cha Knut Musa Nzili amesema liwe liwalo walimu hawatatia sahihi kandarasi ya utendakazi wao hadi serikali iwapandishe vyeo walimu 80,000 ambao tayari wamehitimu kutoka vyuo vikuu humu nchini.

Hii ni baada ya serikali kuwataka walimu kutia sahihi kandarasi ya utendeakazi wao jambo ambalo limepingwa vikali hadi serikali ifanye yale walimu wanahitaji kwanza

Akizungumza siku ya Alhamisi katika shule ya upili ya Kebirigo wakati uchaguzi wa kuwachagua viongozi wa walimu katika chama cha KNUT ulikuwa unafanyika,  Nzili alisema serikali inastahili kusahau sahihi za walimu kati yao na serikali kwani serikali haijafanya yale walimu wanahitaji upandishaji wa vyeo ikiwa moja wapo.

“Walimu wote wameajiriwa na hakuna mambo ya kutia sahihi ya utendakazi wao na serikali, hilo hatutalikubali kamwe,” alisema Nzili .

“Tunataka walimu 80,000 ambao wamehitimu kutoka vyuo vikuu wapandishwe vyeo kwanza na hatutadanganywa na hatutatia sahihi ya utendekazi,” aliongeza Nzili.

Katika uchaguzi huo, Kennedy Nyamwanda alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama cha hicho tawi la Nyamira, Kennedy Migosi alichaguliwa kuwa katibu wa chama hicho, Jared Maangi alichaguliwa kuwa naibu wa mwenyekiti, Bira Bihaji alichaguliwa kuwa mwakilishi wa wanawake miongoni mwa wengine

Nzili alisema uchaguzi huo ulikuwa wa haki na waliochaguliwa watafanya kazi pamoja na chama cha KNUT kufanya mengi.