Share news tips with us here at Hivisasa

Wananchi na viongozi kutoka eneo la Subukia wametoa wito kwa maafisa wa usalama kujitahidi zaidi na kumkamata kijana aliyewaua nyanya na babuye mjini Subukia wiki jana.

Wakiongea nje ya ufuo wa jimbo la Nakuru ambapo walifika kuchukua miili ya marehemu Peter Kaboga aliyekuwa na miaka 90, na Hanna Kaboga wa miaka 85, viongozi hao wakiongozwa na MCA Peter Njoroge Mwanjo wamesema kuwa kutopatikana kwa mshukiwa kungali kunatia wananchi hofu eneo hilo.

Wamemtaka OCPD wa Subukia Alex Ng’ang’a kuongoza zoezi la kumtafuta mshukiwa hata kama italazimu kuomba usaidizi wa maafisa kutoka nje ya eneo lake.

“Wananchi wanaishi kwa hofu ya kuvaamiwa na mshukiwa, kwa sababu hajapatikana na kuna uwezekano hayuko mbali japo alitafutwa hata kwenye vichaka na hakupatikana,” Mwanjo alisema .

Mshukiwa huyo alichimba shimo kando ya nyumba na kuingia chumbani walimokuwa wamelala wakongwe hao Desemba18, 2015 na kuwakatakata.