Sintofahamu ilitanda katika kijiji cha Karima mjini Naivasha baada ya kupatikana kwa mwili wa mtoto wa miaka sita ukielea kwenye bwawa.
Kiasi hicho kilizua wasiwasi mjini humu hukuwenyeji wakitaka uchunguzi kufanywa ili kubainika kwa kilichosababisha tukio hilo
John Kimani, ambaye ni mkaazi, alisema kuwa mtoto huyo aliripotiwa kutoweka Jumatatu wiki jana na wakaazi wamekuwa wakisaidiana na familia kumtafuta.
OCPD wa Naivasha Titus Munyoki alidhibitisha kisa hicho na kusema kuwa polisi watafanya uchunguzi kuhusiana na kisa hicho.
Mwili huo ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya kaunti ndogo ya Naivasha.