Idadi ya miili ambayo haijachukuliwa katika hifadhi za miili katika hospitali za serikali kaunti ya Nakuru inaendelea kuongezeka kila uchao.
Hayo yalijiri huku ripoti zikiibuka kuwa kaunti hiyo ina zaidi ya miili sabini ambayo inafaa kuzika katika kaburi la pamoja.
Shida hiyo imetokana na kutokuwepo kwa ardhi mwafaka ya kutumiwa kama kaburi kutokana na kufungwa kwa makaburi ya umma ya Naivasha na Nakuru, kwa kujaa.
Akizungumza Jumanne, mkurugenzi wa maswala ya afya katika kaunti hiyo Samuel King’ori alisema kuwa mwaka jana pekee walizika miili 200 yote ikiwa kwenye hifadhi za miili za umma katika kaunti.
"Kaunti hii imepoteza mamilioni ya hela katika shughulu ya kuzika miili ambayo imekaa kwenye fuo nyingi za hospitali za umma hapa Nakuru," Alisema King'ori.