Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Muungano wa vijana wa amani katika Kaunti ya Mombasa wameikosoa idara ya mahakama nchini kwa kushiriki ufisadi na wataka mahakimu na majaji kujitenga na ufisadi ili kuwajibikia majukumu yao vyema mahakamani..

Wakiongozwa na kiongozi wa vijana katika eneo la Kisauni mjini Mombasa Maxwell Masai, wakazi hao wamesema kuwa hatua ya mahakama kuchukua muda mrefu kukamlisha kesi zilizoko mahakamani imechangiwa na ufisadi katika idara za mahakama.

Akizungumza na wanahabari katika eneo la Kisauni mjini Mombasa siku ya Ijumaa, Masai amesema kuwa hatua kisa cha hivi majuzi cha jaji wa mahakama ya juu zaidi kuhusika katika kashfa za ufisadi inaonyesha wazi jinsi idara ya mahakama imekosa mpangilio.

Masai sasa anataka jopo la uchunguzi lililobuniwa na Jaji mkuu nchini Willy Mutunga kuwafanyia uchunguzi wa kina na kutoa ripoti mwafaka dhidi ya madai yanayomkumba jaji wa mahakama ya juu zaidi Philip Tunai kuwa alihusika katika kupokea rushwa ya shilingi milioni 200 kutoka kwa Gavana wa Kaunti ya Nairobi Dkt Evan Kidero ili kutupilia mbali kesi ya uchunguzi dhidi ya mpinzani wake.

“Tunataka kuona jopo lililobuniwa na Jaji mkuu kufanya uchunguzi wa kina na kutoa ripoti mwafaka dhidi ya madai hayo kwani ni wazi kuwa gavana wa Nairobi ameshtakiwa kwa kutoa rushwa ili kusaidiwa kusalia katika uongozi na ni wazi kuwa alishindwa,” alisema Masai.