Idara ya polisi imefanya mabadiliko makubwa katika kaunti ya Mombasa ambapo kamanda mpya wa polisi Pwani atakuwa Nicholas Kamwende, ambaye alikuwa mkuu wa upelelezi eneo la Nairobi.
Naye Henry Ondiek, aliyekuwa na nafasi hiyo eneo la Pwani atakuwa afisa wa upelelezi wa jinai katika kaunti ya Nairobi.
Mkuu wa kitengo cha upelelezi wa jinai Mombasa Zachary Nangulu atakuwa mkuu wa kitengo cha upelelezi wa jinai Nairobi, na nafasi yake hapa Mombasa imechukuliwa na Hussein Bakari kutoka Nairobi.
Aidha, mkuu wa upelelezi wa jinai Changamwe Betty Chepng'eno amepelekwa Chuka, na nafasi yake kuchukuliwa na Francis Macharia ambaye amekuwa naibu kamanda wa kitengo cha Flying squad, Nairobi.
Mkuu wa upelelezi wa jinai katika bandari ya Mombasa Ali Bule ameondolewa na kupelekwa Eldoret, na nafasi yake kuchukuliwa na Juliana Nduku kutoka Eldoret.