Share news tips with us here at Hivisasa

Wizara ya usalama wa ndani imetoa picha 11 za waahalifu wa ugaidi, na kuitaka jamii kusaidia idara ya usalama katika kuwafichua magadi hao.

Washukiwa hao ni Abdalla Muumin Abdalla, Abdalla Siraj Marumu, Abdifatar Abubakar Abdi, Isaa Abdalla Ahmed na Anwar Yogan Mok, Suleiman Muhamed, Hussein Said, Mohamed Ali Ahmed, Omar Patroba Juma, Abdikadir Abubakar and Ismael Mohamed Shosi, huku wengi wao wakiwa ni wakazi wa eneo la Pwani.

Hatua hii imetolewa baada ya magaidi watatu kukwepa mtengo wa polisi siku ya Jumatatu katika eneo la Majengo jijini Mombasa.

Mkuu wa polisi eneo la Mombasa Francis Wanjohi amethibitisha kupatikana kwa bunduki mbili, risasi 345 na simu 15 kutoka kwa makaazi ya badhii ya washukiwa hao  eneo la Majengo, jijini Mombasa.

Kulingana na uchunguzi wa kijasusi, watatu hao walikuwa wanapanga kutekeleza ugadi katika eneo la Lamu na Mombasa.

.