Mwanaharakati wa kisiasa Abdul Noor amesema kuwa tume ya uchaguzi ya IEBC ilifeli katika kuwahamasisha wapiga kura, hali iliyopelekea idadi ndogo ya watu kujitokeza kujisajili. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Noor amedai kuwa IEBC haikuweka mikakati ya kutosha kuwahamasisha wakenya juu ya umuhimu wa kujisajili kama wapiga kura. 

 Noor aidha ameongeza kuwa iwapo IEBC ingefanya uhamasisho wa kutosha, basi wangeafikia lengo lao la kuwasajili zaidi ya wapiga kura wapya millioni nne. 

"IEBC inafaa kulaumiwa kwa idadi ndogo ya watu waliojisajili kwa sababu hawakufanya uhamasisho wa kutosha ili kuwachochea watu kujitokeza na kujisajili," alisema. 

"Kuna baadhi ya watu hawakujua kuhusu zoezi la kusajili wapiga kura, na kwa hivo hawangejitokeza, lakini kama IEBC ingewapa ujumbe labda wangejitokeza," aliongeza. 

Noor aidha aliitaka IEBC kuwaajiri machifu na manaibu wao ili kusaidia katika uhamasisho siku za mbeleni.

Photo: Mwanaharakati wa kisiasa Abdul Noor. Amelaumu IEBC kwa kukosa kufanya uhamasisho wa kutosha kuhusiana na usajili wa wapiga kura. JOkata/Hivisasa.com