Huku ikisalia siku mbili tu kabla ya zoezi la kusajili wapiga kura wapya, wakazi wa mtaa wa Rhonda wamerai tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kusongeza mbele zoezi hilo ili kuwapa nafasi kujiandikisha. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Wakiongea siku ya Jumapili, wakazi hao walisema kwamba huenda wakakosa kujisajili kwani muda uliotengwa zoezi hilo ulikuwa mchache mno. 

Aidha, waliongeza kwamba nyakati za kuhudumu kwa wasajili wa tume hiyo ilikuwa finyu mno. 

"Nahofia huenda nikose kusajili kwa sababu sina muda wa kufika kwenye kituo cha usajili kutokana na hali ya kazi yangu. Ningeomba IEBC kusongeza zoezi hili anga kwa wiki mbili," alisema John Kimathi. 

Semi hizo ziliungwa mkono na Charity Wamae, mkazi mwingine aliyeongeza kuwa kusitishwa kwa shughuli hiyo kulingana na ratiba huenda ikafungia nje wanafunzi ambao wamehitimu umri wa kujisajili. 

Zoezi la kuandikisha wapiga kura lilianzishwa Februari 15, huku IEBC ikionyesha waziwazi kwamba huenda ikakosa kuafikia azma yao ya kusajili wapiga kura wapya Milioni 4. 

 Picha: Wasajili wa tume ya IEBC wakisajili mpiga kura kwenye picha ya awali. Tume hilo limeombwa kusongeza mbele zoezi la kusajili wapiga kura.