Tume huru ya mipaka na uchaguzi(IEBC) imetakiwa kuchunguza madai ya watu kujisajili zaidi ya mara mbili katika kaunti ya Nakuru Mwanaharakati wa kisiasa Abdul Noor amesema kuwa kuna baadhi ya raia wanaojisajili katika kituo zaidi ya kimoja.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza jumatatu mjini Nakuru Noor alisema kuwa baadhi ya watu wanafanya hivo baada ya kulipwa na wanasiasa.

"Kuna watu wamesajiliwa katika zaidi ya kituo kimoja na wanafanya hivo baadaye ya kulipwa na wanasiasa," Noor alisema.

"IEBC inafaa kuyachunguza na kuwakamata hapo watu waliojisajili mara mbili kwa sababu ni hatia kulingana na sheria za IEBC,"aliongeza Watitu.

Hata hivo mshirikishi wa IEBC eneo lA Central Rift David Towet alisema kuwa hawajapokea madai hayo lakini watachunguza .