Kiongozi wa waliowengi katika bunga la kitaifa Aden Duale ameitaka tume ya IEBC kuhakikisha uchaguzi mdogo wa Malindi ni wa uwazi na wa haki.
Akizungumza huko Malindi siku ya Jumatatu, Duale alisisitiza haja ya kuweko kwa kura zenye uwazi, haki na zenye amani ili kupatikane viongozi bora kwa wananchi.
Duale aliwataka wapiga kura kujitokeza kwa wingi na kuwachagua viongozi wanaowapenda.
Aidha, alisisitiza kuwa Jubilee imejitenga na siasa za matusi na chuki kwa jamii.
Duale aliyasema haya baada ya kushuhudiwa joto la kisiasa la uchaguzi mdogo huko Malindi.