Serikali imetakiwa kutenga fedha zaidi Kwa Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC, kuelimisha wananchi kuhusu zoezi la upigaji kura.
Akizungumza siku ya Jumatatu, mwanasiasa Johnson Kinyanjui kutoka eneo la Njoro alisema kuwa idadi ndogo ya wakaazi wanajitokeza kusajiliwa kutokana na kutoelimishwa.
"IEBC inafaa kutengewa fedha zaidi ili waweze kuelimisha wananchi kuhusiana na maswala ya upigaji kura,” alisema Mwamba.
Hata hivyo, mwanasiasa huyo alitoa wito kwa wakaazi wa Njoro kujisajili kwa wingi kama wapiga kura ili kushiriki uchaguzi mkuu ujao.
Kinyanjui alisema kuwa kwa miaka kadhaa, eneo bunge la Njoro limesalia nyuma kwani viongozi wanaochaguliwa hawajali maslahi ya mwananchi wa kawaida.
Kinyanjui ametangaza azma ya kuwania kiti cha eneo bunge la Njoro katika uchaguzi mkuu wa 2017.