Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanaume mmoja wa umri wa makamo alifikishwa mbele ya mahakama ya Nakuru Alhamisi na kushtakiwa kwa kosa la kupatikana na kilo zaidi ya 300 za nyama mwitu.

Mbele ya hakimu Doreen Mulekyo, mshukiwa huyo alidaiwa kuingia kwenye mbuga ya wanyama ya Nakuru na kuwaua wanyama kadhaa kwa minajili ya kutoweka na minofu yao.

Upande wa mashtaka ulitoa kilo kadhaa za nyama hiyo mahakamani kama ushahidi dhidi ya mshukiwa.

Kulingana na upande wa mashtaka, Joseph Kamau alitiwa mbaroni siku ya Jumanne na maafisa wa hifadhi ya wanyama pori KWS kwenye mbuga hiyo.

Kamau alikanusha mashtaka hayo na kuachiliwa kwa dhamana. Kesi hiyo itaskizwa Machi 3.