Jamaa mmoja aliuawa baada ya kudaiwa kupatikana peupe akiiba kuku.
Mwanamme huyo mwenye umri wa makamo ambaye kulingana na chifu mkuu wa kata hiyo Francis Kariuki alikuwa na kreti mbili za kusafirisha kuku hao kwa baiskeli.
Umati ulioitika kamsa ya mwenye kuku hao mwendo wa saa tisa usiku wa kuamkia Jumatano, ulimpatiliza kichapo cha haja mshukiwa huyo baada ya kususia kutaja wenzake, katika wimbi jipya la uhalifu wa aina hiyo.
“Alikataa kabisa kusema jina lake, lakini akasema kwamba anatoka Kaptembwa na ana bibi na watoto wawili,” mkaazi alisema.
“Hatukujua jina lake lakini alikuwa na stakabadhi zilizoonyesha kwamba anatoka Kaptembwa, na pia simu yake ilikuwa na nambari za simu za wateja wake wa hoteli Kaptembwa,” chifu Kariuki alisema.