Jamaa mmoja anayedaiwa alikuwa akivuna viazi kwenye shamba la jirani aliuawa siku ya Jumatano baada ya kufumaniwa kwenye shamba hilo.
Chifu wa Molo Hassan Waweru amedhibitisha kisa hicho.
Waweru amesema mshukiwa huyo ambaye alitambuliwa kama John Gachie alipatikana asubuhi na mapema kwenye shamba hilo katika eneo la Kapsita.
“Alipatikana kwenye shamba hilo akichiba viazi,” Waweru alisema.
Aidha Waweru alisema kisa hicho kilitokea alfajiri saa kumi na mbili.
“Mlinzi wa shamba hilo alimpata mwendazake na kumpatia kichapo na kifaa butu hadi kufariki,”Aliongeza Waweru.
Chifu Waweru amesema kuwa kisa hicho kinachunguzwa na polisi.
Amewataka wananchi kutochukua hatua mikononi mwao bali washukiwa wafikishwe mahakamani ili kuadhibiwa kwa mujibu wa sharia.