Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mahakama ya Mombasa imemfunga kifungo cha miaka minne gerezani kijana wa umri wa makamo aliyepatina na kosa la wizi wa gari.

Kati ya Septemba 2, 2011 na Octoba 19, 2011 katika maeneo yasiyojulikna jijini Mombasa, Gaya Joseph anadaiwa kuiba gari aina ya Mitsubishi Pajero yenye thamani ya shilingi 1,127,760, ambayo ni mali ya kampuni ya Mwamba Freight Services Limited.

Akitoa uamuzi huo siku ya Jumanne, hakimu katika mahakama ya Mombasa Richard Odenyo alisema kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa, mshukiwa alihusika katika wizi huo.

Aidha, Odenyo aliongeza kuwa hukumu hiyo itakuwa funzo kwa wengine wanaotekeleza wizi kote nchini.

Wakati huo huo, bibi na watoto wa mshukiwa huyo walitokwa na machozi baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, ishara tosha kuwa uamuzi huo uliwathuru pakubwa.

Aidha, kutokana na huzuni, familia hiyo ilikataa kuzungumza na mwanahabari huyu.