Mtu mmoja aliuwawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa KDF katika eneo la Dona Olinda Mtongwe alfajiri ya Alhamisi baada ya kudaiwa kurushia mawe gari la maafisa hao walipokuwa wakipita.
Wakaazi wa eneo hilo walioshuhudia kisa hicho walisema kuwa marehemu alikuwa na akili punguani.
Kamanda wa polisi eneo la Likoni Willy Simba alithibitisha kisa hicho na kusema kuwa uchunguzi umeanzishwa kuhusiana na kisa hicho.
Simba alisema marehemu alipigwa risasi moja ya tumbo.
Mauaji hayo yalizua hisia kali miongoni mwa wanaharakati wa haki za binadamu wakiyataja kama mauaji ya kutamausha.