Jamii ya wahindi ambao watasherehekea siku kuu ya Diwali mnamo siku ya Jumamosi wamehakikishiwa usalama wakati watakapokuwa wakiadhimisha siku hiyo kwenye eneo la Mombasa Sports Club eneo la Mbaraki, jijini Mombasa.
Kwenye kikao na waandishi wa habari kwenye ofisi yake, naibu wa kamishna wa Kaunti ya Mombasa Mohammed Salim, alisema kuwa idara ya usalama itaweka usala wa kutosha huku sherehe hizo zikifanywa Jumamosi.
Aliwataka wananchi kutobabaika watakaposikia baruti zikirushwa hewani kwa sababu iyo ndiyo mojawapo ya njia ya waumini hao wa Hindu wanafanya maadhimisho yao, na kuwasihi wakazi kutofanya mambo ambayo ni kinyume na sheria nyakati zote kuwa makini na kufuata sheria.
Alionya kuwa serikali kupitia idara zote za usalama zitakuwa macho huku akisema kuwa kuna wahalifu ambao hujihusisha na maovu nyakati muhimu kama hizo.
“Wananchi wakisikia fataki wasifadhaike kwani wenzetu wa jamii ya Hindu watakuwa wanasherehekea siku yao, na kuna wale watakuwa wanarusha fataki zao lakini jua kuna utaratibu wa kufanya sherehe hiyo na sherehe hiyo itakuwa saa kumi nambili jioni hadi saa sita usiku siku ya Jumamosi,” alisema Salim.
Wataki huo maalum wa wahindu unasherehekewa kila mwaka kwa kurusha fataki hewani, na ni miongoni mwa maadhimisho ya dhehebu hilo ambayo ni maarufu zaidi ambapo wanasherehekea mazuri ambayo yametokea dhidi ya maovu kwa kurusha fataki.