Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwakilishi wa kina mama kaunti ya Trans Nzoia Janet Nangabo ameishauri jamii ya waluhya inayoishi Nakuru kuhakikisha wameingia serikalini ifikapo kinyanganyiro kijacho cha mwaka wa 2017.

Amesema kuwa jamii yao haitaelekezwa kamwe na baadhi ya viongozi wachache ambao ushindi wao katika uchaguzi ujao uko duni.

Akiongea mjini Nakuru siku ya Jumatatu, Nangabo aliwataka wafuasi wa chama cha Ford Kenya na wale wa New Ford Kenya anaodai wana kura nyingi kutoka jamii ya Abukusu, kuungana pamoja na kuunga muungano wa Jubilee mkono.

Amesema kuwa wale walio na tashishwi na muungano huo hawasemi bayana, huku akidai kuwa vyama vidogo vidogo havina uwezo wa kuuunda serikali na vilevile iwapo hawataunga jubilee mkono watasalia kwa upinzani.

“Jamii ya Abukusu ilisalia upinzani wakati wa serikali ya Kanu na huenda wakapelekwa huko na viongozi wanaojipenda,” Nangabo alisema.