Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Katibu mpangaji wa muungano wa vyuo na taasisi eneo la Pwani Abubakar Swabir amewataka wakazi wa Pwani kushirikiana ili watoto wa mtaani wapate malezi bora na kuepuka vishawishi na kujiunga na makundi ya vijana ya kigaidi.

Akizungumza katika maadhimisho ya maandilizi ya kusheherekea sherehe za Krimasri na familia za wanaolala mitaani siku ya Jumatatu, Swabir alisema kuwa ushirikiano huo utawasadia watoto wasio na makao kuepuka vishawishi katika utendaji wa uhalifu, na kujihisi kama watoto wengine wanaopata malezi bora kutoka kwa familia zao.

Aidha waziri wa vijana, jinsia na michezo Kaunti ya Mombasa Mohammed Abbass amewataka vijana kujiunga na makundi mbali mbali ili kufaidi kutokana na mikopo katika miradi ya ugatuzi ili kupungza uhalifu katika Kaunti ya Mombasa.

Kulingana na Abbass, iwapo vijana wa mtaani hawatashirikishwa katika maswala mbali mbali, huenda wakazidi kujihusisha katika uhalifu ili kujikimu na maisha na kuzorotesha pato kutoka kwa watalii nchini.

Vilevile Abbas amewataka wazazi kuwapa malezi bora watoto wao ili kupunguza idadi ya watoto wa mitaani barabarani.

Hata hivyo, familia za wanaolala mtaani wamekiri kuwa maafisa wa usalama wa Kaunti ya Mombasa huwashika ns kuwapeleka korokoroni licha ya kutofanya uhalifu wowote.

Kulingana na familia hizo, ukosefu wa makao umewafanya kulala nje na sio uhalifu kama wanavyodhania maafisa wa usalama wa kaunti.

Vile vile, familia za wanaolala mitaani zimeitaka serikali kuwapa makao ili kupunguza visa vya ubakaji miongoni mwa wasichana na watoto wadogo wanaoishi mitaani.

Itakumbukwa kuwa watoto wa mitaani walishiriki katika maadhimisho ya watoto wa mitaani mapema mwaka huu ili kuhakikisha serikali imetatua baadhi ya changamoto wanazopitia ikiwemo kupata makao ili wapate malezi bora kulingana na hakikisho katika katiba nchini.