Wanawake na wanaume wa karne hii ya leo wamekumbatia sana uchubuaji wa ngozi na kutamani kuwa weupe zaidi ya walivyoumbwa. 

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wengi wao wanasema kuwa ni kidijitali huku wengine wakisema kuwa watu weupe ndo hupendwa sana na huonekana kuwa 'matajiri'. 

Hayo kando, je wazijua athari zake? 

Kwanza unapochubua ngozi yako, huenda ukaugua saratani ya damu kufuatia kemikali iliyoko kwenye mafuta hayo. Pia kemikali hizo huchoma ngozi na kuua madini muhimu mwilini. Hii huhatarisha maisha ya mwenye kutumia mafuta hayo kwani huongeza uwezekano wa kupata saratani ya ngozi pia.

Kemkali iliyoko katika mafuta haya husababishia wanawake wajawazito kujifungua watoto ambao hawajakamilika kimaumbile. Mara kwa mara pia utumizi huo husababisha ngozi kuwa nyepesi sana na hata kutatiza shughuli ya kushonwa mtu anapofanyiwa upasuaji. 

Pia kuna magonjwa mengine kama vile ya figo yanayoletwa na matumizi ya mafuta haya.

Yote tisa, kumi ni kuwa kuna njia mbadala za kupata ngozi 'nyeupe' kama vile kunywa maji mengi kwani maji hunawirisha afya, kula lishe bora ili mwili uongeze madini na kutumia maji ya malimau unapokoga kwani citric yaondoa madoa doa ya makovu mwilini. 

Chaguo ni lako na jibu unalo.