Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kinyume na kaunti nyingi nchini, kaunti ya Mombasa ni Kaunti iliyo na maajabu mengi na mambo mengine ya kufurahisha mno.

Kwa fahamu ya wenyeji na sintofahamu ya wageni makala haya yangependa kukufahamisha na kukuweka wazi kile hujawahi jua ni kuwa majina ya  mitaa mingi inayounda kaunti ya Mombasa yanaishia kwa ‘ni’.

Ukweli ulio wazi ni kuwa mitaa hiyo pia ina maana ya majina hayo ambayo mengi husawiana na kilichofanyika mahali hapo au kilichopandwa eneo hilo.

Orodha inayofuata inathibitisha haya madai;

Likoni – huu ni mtaa unafahamika zaidi kutokana na kuwa na kivuko cha feri na neno lenyewe linatokana na nomino Liko ambayo humaanisha Bandari.

Ganjoni – ni mtaa ulio katikati ya jiji la Mombasa na wengi wa wakazi eneo hilo huaminika kuwa wenye pesa na hutokana na neno Ganjo ambalo humaanisha mahame yaani mahali hamna wakazi au watu wanaoishi mahali hapo ni wachache. Inaaminika kuwa eneo hilo halikuwa na watu wengi mwanzo mwanzo mwa karne ya 1900 kufuatia kuhama kwa watalii walioishi hapo.

Miritini – mtaa ulio nje ya jiji la Mombasa na huwa la makazi ya watu wenye kipato cha kadri; hutokana na neno mriti/miriti aina ya miti ambayo magome yake hutengenezwa kamba na hutumiwa kwenye ujenzi na imewahi kustawi eneo hilo.

Vijiweni – kijiji kwenye mtaa wa Mtongwe-kutokana na vijiwe vidogo vidogo vilivyotumiwa kujengea.

Bondeni – eneo kati ya jiji la Mombasa ambako ndiko mna soko maarufu la Marikiti - kutokana na bonde

Ngomeni – mtaa ulioko nje ya Mombasa na sehemu kubwa iko Kilifi inaaminka kuwa kulijengwa ngome yaani nyuta za kukinga adui pamoja na kuenea kwa maji ya bahari kuingi majumbani.

Orodha ni kubwa miji mingine ni pamoja na

Mikindani – mtaa mmoja unaokuwa kwa haraka nje ya jiji na neno hilo hutokana na mkinda aina ya ngoma.

Kibokoni – mtaa katikati ya jiji la Mombasa neno hilo linatoka kwenye nomino aina ya mnyama kiboko.

Mikanjuni- kutokana na aina ya mti (Mkanju/mikanju) unaozaa mabibo(yaani korosho)

Kiembeni, Kombani, Kisimani, Shimoni n.k.

Naamini kuwa umejifunza.