Mapumbu ni aina ya maradhi ambayo mara nyingi yamekuwa yakiwaathiri wakazi wa eneo la pwani ya Kenya.
Hata hivyo kuna sababu nyingi zinatajwa kuwa chanzo kikuu cha maradhi hayo kuwalenga wakazi wa eneo la pwani huku wenyeji wakiamini kuwa maradhi hayo yanahusiana na ushirikina kauli ambayo inakinzani wima na mtazamo wa waatalam wa tiba na wanasayansi kwa jumla.
Mapumbu uvimbe kwenye korodani yaani sehemu ya uume hasa huwaathiri wanaume kwenye mshipa unaunganisha kiungo cha uzazi cha mwanaume ambapo mshipa huo unavamiwa na virusi vinavyosababisha maradhi hayo husababisha uume kufura.
Yafutayo ni baadhi ya mitazamo mseto kuhusiana na kinachochangia na kusababisha ugonjwa huu ambao upo kati na miongoni mwa maradhi ogopewa kwa wenyeji.
Wenyeji Mombasa – baadhi ya wakazi katika kaunti ya Mombasa wana imani kuwa maradhi haya husababishwa na joto kali ambalo lipo katika maeneo ya pwani
Wengine wanadai kuwa maradhi hayo husababishwa na hunywaji wa aina ya majimaji yanayotokana na tunda maarufu katika maeneo hayo la Madafu.
Hayo yasitoshe kuna wale bado wameshikilia msimamo kuwa mapumbu huletwa na watu wa kishirikina na hasa walio na roho mbaya ya kutowatakia wenzao kuendelea kimaisha.
Hata hivyo madai hayo kwa mara si moja yamekanwa na wataalam wa masuala ya matibabu wakisema kuwa hayo ni maradhi kama maradhi mengine na mara nyingi utafiti umeonyesha kuwa huletwa na virusi Fulani ambavyo uvamia mishipa ya kuunganisha sehemu za uzazi za wanaume na wahusika ufanyiwa opereshini kuondolewa kupata tiba.
Sababu ya kuwavamia wanaume pekee bado haijabainika.