Share news tips with us here at Hivisasa

Gavana wa Kaunti ya Mombasa Hassan Joho ametakiwa kuchukua jukumu la kuwasimamisha kazi maafisa wa serikali ya kaunti hiyo wanaoshiriki ufisadi ili kulinda mali ya umma.

Kulingana na Kiongozi wa Vijana katika eneo la Kisauni Maxwell Masai, baadhi ya idara mbalimbali katika kaunti hiyo zimeshindwa kuendeleza shughuli za kimaendeleo kwa wananchi kufutaia kukithiri kwa ufisadi.

Akizungumza katika eneo la Kisauni mjini Mombasa siku ya Ijumma, Masai alisema kwamba tangu serikali ya kaunti kuchukua uongozi, wakaazi hawajafaidika kutokana na utumizi mbaya wa raslimali na fedha za umma.

Aidha, Masai amemshikiza Gavana Joho kuwachunguza maafisa wakuu wa idara mbalimbali katika serikali ya kaunti na kuwasimamisha kazi walio wafisadi kwani wanazidi kudidimiza maendeleo.

“Tunamtaka gavana wa kaunti hii ajitokeza wazi na kufuta kazi maafisa wafisadi ili kuwezesha shughuli za kimaendeleo kunawiri, kwa sababu kuna baadhi ya maafisa wanafuja fedha za umma na kuwaacha wananchi wakiwa na maisha magumu,” alisema Masai.