Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho amemlaumu Rais Uhuru Kenyatta kwa kuzuru Mombasa bila ya kumjulisha ikizingatiwa kuwa yeye ndiye rais wa kaunti.
Akizungumza mbele ya rais huko Shika Adabu, Joho alimweleza rais kuwa alivyofanya sio sawa, na kumtaka rais kulirekebisha hilo ili wafanye kazi kwa umoja licha ya tofauti zao za kichama.
Ilimlazimu gavana huyo kumkumbusha rais kuwa katika kaunti nyengine anazokwenda hukutana na magavana, ila wakati huu ameamua kumtenga.
Wakati akisema hayo, Rais Uhuru alikuwa akimsikiliza kwa makini huku baadhi ya wananchi wakimuunga mkono kwa shangwe.
Wakati huo huo, Seneta wa Nairobi Mike Mbuvi naye amemlaumu Gavana Joho kwa madai kuwa hana ukaribu na Rais Uhuru Kenyatta, ndio maana hakuhusishwa wakati huu rais Uhuru alipozuru Mombasa .
Mbuvi pia alilaumu upinzani kwa kukosoa serikali wakati wao walijuhusisha na ufisadi na unyakuzi wa ardhi.