Share news tips with us here at Hivisasa

Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho amepongeza hatua ya serikali ya Marekani ya kuondoa vikwazo vya usafiri kwa raia wake humu nchini.

Joho ameyazungumza haya siku ya Jumanne baada ya kumpokea balozi wa Marekani humu nchini Robert Godec katika jumba la makavazi ya kitaifa la Fort jesus mjini Mombasa.

Alisema kuwa kuwepo kwa balozi huyo katika kaunti hiyo kunaashiria kuwepo kwa utulivu, na kuongeza kuwa jiji la Mombasa ni salama humu nchini na katika ngazi za kimataifa.

Naye mbunge wa mbunge wa Mvita Abdulswammad Sharrif Nassir amepongeza ushirikiano baina ya serikali ya kaunti ya Mombasa na Marekani.