Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Joho ametoa wito kwa rais Uhuru Kenyatta kumpa uhamisho mshirikishi wa kanda ya Pwani Nelson Marwa kwa maadai kuwa Marwa amekua akipinga uongozi wa kaunti hiyo.

Akizungumza na wanahabari, Joho alisema kuwa kama mkuu wa usalama, Marwa hapaswi kuwa anaunga mkono mrengo wowote wa kisiasa licha ya kuwa alichaguliwa na Rais katika nyadhfa hiyo.

Viongozi hao wamekuwa na malumbano siku zilizopita jambo ambalo limeonekana kuchochea kuondolewa kwa walinzi wa Gavana Joho na wakuu wa polisi katika kaunti ya Mombasa.

Walinzi hao waliondolewa baada ya Marwa kusema kuwa angewachukulia hatua kwa kuzembea kazini katika uchaguzi mdogo wa Malindi.