Share news tips with us here at Hivisasa

Serikali ya Kaunti ya Mombasa imemtaka Rais Uhuru Kenyatta kuondoa ada itakayotozwa wakazi wa shamba la waitiki jijini Mombasa.

Kauli hii ilitolewa na Gavana wa Mombasa Hassan Joho kwa kusema kuwa ada hiyo ni ya juu ikilinganishwa na mapato duni ya wakazi wa eneo hilo.

Aidha, Bw Joho alisisitiza kuwa ni jukumu la serikali kuwapa wananchi ardhi hiyo bila kuwatoza ada yoyote.

Hatua hii inajiri baada ya Raisi kusema kuwa pesa alizolipwa mmiliki wa shamba hilo Evans Waitiki zilitoka katika hazina ya makaazi ambayo ni sheria pesa hizo kurudishwa ili kutumia tena katika ardhi yenye utata.

Hata hivyo Kenyatta alisema kuwa serikali kuu iko tayari kufanya maongezi na serikali ya Kaunti kuondoa gharama hizo kwa mwananchi au wananchi hao kuongezewa muda hadi miaka kumi na mbili kumaliza kulipa.

Itamlazimu kila mwananchi kulipa shilingi 180,000 ilikupata kipanden cha ardhi hiyo.