Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Huku kukizuka malumbano kati ya chama tawala cha Jubilee na kile cha upinzani Cord kuhusiana na uhalali wa mgombezi wa kiti cha ubunge cha Malindi, Willy Mtengo, Gavana wa Mombasa amewataka wakazi kutotishwa na uzushi huo na kuwataka wenyeji kujitokeza wakati wa kura kumpigia kura mgombea huyo wa Cord.

Akiongea katika hafla ya kuendeleza kampeni za muwaniaji huyo, Gavana Ali Hassan Joho amesema kuwa wana imani kuwa chama chao kinahifadhi kiti hicho, na kutaja madai hayo kuhusiana na elimu ya Mtengo kuwa ni mbinu tu ya viongozi wa Jubilee ambapo wanatafuta kusingizia ili kupata uungwaji mkono kutoka kwa wapiga kura.

Joho ambaye ni mkosoaji mkubwa wa serikali ya upinzani alisema kuwa sharti wapiga kura kutoka eneo la Malindi kuwa na imani na chama chao.

Kwa upande wake mgombeaji ambaye atapeperusha bendera ya muungano huo Willy Mtengo amejitetea kwa kusema kuwa ana vyeti vya masomo halali na anapita viwango vigego hitaji vya kusimama kiti chochote hata cha urais.

Mtengo watakabiliana na mgombeaji wa chama cha Jubilee Philip Charo, na tayari viongozi wengi wa vyama vya upinzani na wale kutoka upande wa serikali wakiwafanyia kampeni wagombea husika.

Kiti cha Malindi kiliachwa wazi na Dan Kazungu kufuatia kuteuliwa na rais Uhuru Kenyetta kuchukua hatamu ya wizara ya madini.